MOJA KATI YA MASHAILI MZURI.
1.Mke mwema utulivu, hili halina UbishiAnakutoa machovu, ya kazini kama moshiHana chembe ya uvivu, kila kitu hash hashiMke mwema utulivu, ndio raha ya dunia.
2. Ni raha juu raha, nyumbani ukibakiaWala hamna karaha, bashasha hunawiriaHuna haja ya kuhaha, baridi roho hukaaMke mwema utulivu, ndio raha ya dunia
3. Kidogo kwake chatosha, hakuna kudangadangaNa hakuna mshawasha, hata upande wa kangaMahaba hunawirisha, japo kibaba cha ungaMke mwema ni neema, ndio raha ya dunia.
4. Na munapoambizana, hukaa na kusikiaHafanyi hata kuguna, ishara ya kuchukiaNyuso zina ng'ara sana, na watu huulizanaMke mwema ni neema, ni fahari ya dunia.
5. Na mume awa hakongi, majirani hushangaaKwa nini jamaa dingi, a shine na kung'aaSiri chini ya mtungi, hataki hata umbeaMke mwema ni neema, ndio pepo ya dunia,
6. Na hapendi vijishoga, mara huku mara kuleNa hana muda wa soga, kila siku yuko mbeleHapendi kuigaiga, kila kitu kwa sumileMke mwema rah a sana, kila mtu alijua.
7. Na hata kwenye kibanda, mutaishi kwa muruaNa japo kupanda punda, msimamo hushikiaHakuna kupinda pinda, na nyuma kufikiriaMke mwema ni neema, mola akikujalia.
8. Utulivu huwa moyo, si mali wala magariWangapi waliyonayo, kukicha haweshi shariAsubuhi wenda myayo, usiku kucha ngangariMke mwema ni neema, Muume akiwa nayo.
9. Tabia haifundishwi, mtu hujengeka nayoNa mtu hababishwi, hiyo huwa mwenendoyoNi vibaya havipishwi, nafsi huwa na choyoMke mwema ni neema, kiumbe ukiwa nayo.
10. Kukicha yananawiri, miaka nenda ishapitaWala husikii kwiri, hutembea na kunyataShamsham bila shari, wajukuu washapataMaisha huwa matamu, mke mwema kuwa nae.
11. Na ukipata mkorofi, atakutoa kiparaKukicha hwishi makofi, na hakuna masikharaHugombana na mawifi, ajae humchararaMke mwema ni neema, na ni raha ya dunia.