Angalia picha mbalimbali za makundi ya dini za Kikristo na kiislamu kama yalivyonaswa na jicho la GK wakiwa katika bustani maarufu ya Hyde park jijini London nchini Uingereza, yakivuta mamia ya makundi ya wapita njia ambao walikuwa wanaingia katika bustani hizo kupumzika na kuota jua.
Ambapo makundi hayo kila mmoja alikuwa akihubiri kuhusu kile anachoamini kuhusu dini yake, ambapo katika mihadhara hiyo ambayo hufanyika kila siku za jumapili, katika siku ya jumapili ya jana ilivuta mamia ya watu kutokana na hali ya hewa jijini London kuwa ya joto kiasi kutokana na kuwepo kwa jua. ama kweli Mungu nimkubwa sana jamani.