Tawi la CHAVITA Mtwara kwa kifupi CHAVITA MTWARA lilianzishwa mwaka 2001 chini ya Katiba na kanuni za Matawi ya chama cha Viziwi TTanzania (CHAVITA) kwa juhudi za Viziwi wenyewe. Pia sawa na Matawi yote ya CHAVITA Tawi linatumia nembo na Kauli mbiu ya CHAVITA ambayo ni USAWA NA HAKI. Aidha Tawi linatumia Dira na Utume wa CHAVITA katika kutekeleza malengo yake.DIRA.
CHAVITA itahakikisha kwamba jamii ya Watanzania inawatambua,inawakubali,inawathamini,inawashirikisha Viziwi na kuhakikisha hawasumbuliwi na umasikini,unyanyasaji,ubaguzi na ukandamizaji wa aina yoyote.UTUME.
CHAVITA itahakikisha kwamba Jamii ya Viziwi ina Maisha bora,inajijengea uwezo wa kujiamini,kujiendeleza,kukuza lugha ya Alama ya Tanzania na kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za kimaendeleo,kiuchumi na kijamii kwa kushirikiana na Serikali na Taasisi zingine.