Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

LADY JAYDEE AELEZA SABABU ZA KUJIFUNZA KARATE...ANATAKA KUMKABILI NANI? BOFYA HAPA UMSIKILIZE

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Moja kati ya surprises zilizokuwepo wiki iliyopita ni pamoja na habari ya Lady Jay Dee aka Anaconda kujifua kikomando kuumudu mchezo wa Karate, habari iliyoambatana na picha zikimuonesha akifundishwa mchezo huo tena akiwa ndani ya mavazi rasmi.

Itakuwaje Jide akishakuwa fiti kwenye mitindo hatari ya karate kama Shotokan, Wado-ryu, Shito-ry na Goju-ryu? Na je, anataka kumkabili nani hasa? Haya ni kati ya maswali ambayo wengi tulijiuliza. Moko Biashara aka One B wa 100.5 Times Fm alimtafuta Lady Jay Dee na kutuwakilisha kwa kumuuliza maswali hayo nae akafunguka. “Kwa sababu ninao muda wa ziada, halafu kukaa tu idol bila kufanya kitu saa zingine inaweza kupelekea mawazo yako kufikiria vitu vibaya.

Kwa hiyo nikaona sio vibaya nikifanya mazoezi.” Alisema Lady Jay Dee aka Anaconda. Alipoulizwa kama kuna mtu anataka kupigana naye alisema hakuna mtu ila anajiweka fiti tayari kwa lolote. “Hapana ni kutaka kujiweka fiti unajua kufanya mazoezi sio kwa ajili ya kutaka kupigana na mtu, ni wewe mwenyewe tu uwe vizuri ili jambo likitokea ujue jinsi ya kuji-protect.” Ameeleza.

Mkali huyo wa Joto Hasira amedai kuwa ana mwalimu mzuri na kwamba yeye pia ni mwanafunzi mwenye bidii. “Ni mwanzo tu lakini mimi mwenyewe ni mwanafunzi mwenye bidii, bidii yako pale ndio itakayokufanya uweze ku-improve kwa muda mfupi.” Lady Jay Dee alimwambia Moko Biashara aka One B.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top