Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

JITIBU MWENYEWE UGOJWA WA KICHOMI

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
VIJANA wengi leo wanapatwa na maradhi ambayo zamani yalikuwa yanawapata wazee au watu wa makamo. Maradhi hayo ni kama kisukari na mstuko wa moyo.

Kichomi: ni moja ya dalili za ugonjwa wa moyo. Kupatwa na kichomi mara moja moja si vibaya. Bali itakuwa tatizo kama utakuwa ukipatwa muda mrefu au kila wakati. apo unashauliwa kumuona daktari.

Kichomi kinaweza kuwa.
1.Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi kubwa sana (acid) kuzidi kiwango kinacho takiwa mwilini.

2.Dalili ya ugonjwa wa moyo ambao kitaaramu huitwa Ischemic.

Jambo la kuangalia ni je?
1.Unashikwa kichomi ukiwa unatembea?
2.Umeinama au umelala?
3.Ukishakula chakula au baada ya kunywa maji?


 (a) Kama unapatwa na kichomi wakati ukiwa unatembea au ukiwa unashafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo.

(b) Kama unapatwa na kichomi baada ya kula, ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid (uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari (spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimeng’enyui sawasawa chakula kinachokuwa kimeingizwa tumboni, jambo ambalo usababisha mashine ichoke kusaga chakula.

Kawaida binadamu unabidi kubadilisha mfumo wa ulaji wa chakula kulingana na mazingila uliyopo. Usirudie vitu fulani fulani kila siku au mala kwa mala. Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo.

Tatizo jingine ni ulaji wa chakula chenye chumvi nyingi sana, au chumvi yenye kuzidi kiwango cha kawaida katika chakula au kwenye mboga. Chumvi inakorofisha pia mzunguko wa damu mwilini.

Hasa kama hunywi maji ya kutosha kila siku. kwa kawaida binadamu anatakiwa kunywa maji yasiyo pungua lita 4 hadi 6 kwa siku moja. kwaiyo hatuna budi kunywa maji ya kutosha ili kuondokana na tatizo hili.

Kama unapatwa na kichomi ukiwa umelala au umeinama, ina maana kuna tatizo pia la mzunguko wa damu ndani ya moyo au kwenye njia ya mzunguko wa damu inayokwenda kwenye moyon. 

 au labda una tatizo la unene (je unafanya mazoezi ya kutosha?)
kama unafanya mazoezi, je unafanya mazoezi ya aina gani?

Kuna mazoezi ya aina mbili. ni vyema watu mkalitambua hili kwanza.

1. Mazoezi ya nguvu na haraka (cardio vascular);
mazoezi ya namna hii yanaweza kuwa kama kukimbia, kucheza mpira, kupigana ngumi, kuinua vyuma vizito, nk.


2. Mazoezi laini yanayofanywa kwa kukihimili (isometric);
 hapa naongelea mazoezi kama kuweka mkono upande mmoja wa kichwa huku ukisukuma kichwa kisukumane na mkono, unafanya tizi la kuongeza nguvu ya shingo. Zoezi aina hii linaitwa Isometric. na mazoezi mengineyo mengi yenye mfanano wa namna hii. Aina ya mazoezi ya aina hii ni kama Yoga, Pilates na baadhi ya mitindo mbalimbali ya mapigano yaani masho ati mathalan Tai Chi ya Kichina.


Ni muhimu kuchanganya mazoezi  mawili. Yaani ukishafanya mazoezi ya kutumia nguvu (kuhema),  nivyena ukamalizia kwa kufanya mazoezi ya kutulizana, ili kuuwekamwili katika khali ya usawa.

Kama una kichomi cha mara kwa mara yaweza kuwa ni dalili za ugonjwa wa moyo, kisukari au mambo mengine. ili Kuondokana na mambo haya ni vyena ukawai kwenda:

1.Kumwona daktari wa moyo 

2.Kama huna ugonjwa wa moyo angalia unavyokula. Je, unakula sana vyakula vya mafuta?

3.Punguza ulaji wa mafuta au vyakula vizito jaribu kula zaidi samaki ambao huwa na mafuta yasiyoumiza mwili. 

4.VITUNGU SAUMU VIBICHI vinasaidia sana kukinga moyo, matatizo ya mafuta, lakini tatizo la vitunguu swaumu uwa na harufu mbaya ya mdomo. Hivyo unaweza kuwa unachanganya na mboga nyingine za saladi unapokula au kitu chochote kile ambacho kitaweza kupunguza harufu iyo, unaweza kuchanganya na nyanya, matango, nk ukawa unakula kila siku hadi mda wa siku 7 hadi 14.

Mbali na ulaji suala la mapumziko ya kutafakari au kitaaramu tunaita Meditation limefanyiwa utafiti na kuonekana kwamba linasaidia sana maradhi ya moyo, akili na “stress” ya mwili kwa ujumla. Jaribu njia hizi hapa chini, ukiweza dakika kumi hadi 20; mara mbili kwa siku, kufuatana na muda ulio nao.

1. KUKAA TU
2. KUVUTA PUMZI
3. KULALA CHALI HUKU UNAVUTA NA KUPUMUA, hii ni aina ya masho ati ya Kirusi ambayo inasisitiza Uvutaji pumzi sahihi. endapo utafuata masharti na kufanya mazoezi vizuri, basi utakuwa umejiweka katika nafasi nzuri ya kuondokana na tatizo ili la kuumwa au kushikwa na kichomi.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top