Kila mwanadamu hususan wale walioko katika mahusiano, hufurahia sana pale kunapokuwa na dalili za kuitwa baba au mama, kwa maana zinapokuwepo taarifa za mwanamke kuwa mjamzito.
Hata hivyo, furaha hizi mara kadhaa pia zimekuwa zikiishia kuwa machungu baada ya ujauzito kuharibika. Hata hivyo, masikitiko mengi yatokanayo na kuharibika kwa ujauzito, yanaweza kuepukika kama tu watu tutafahamu baadhi ya mambo ya msingi ambayo tunatakiwa kuyazingatia wakati tunapokuwa na mzazi mtarajiwa katika sehemu tunazoishi.
Na hapa, ni baadhi ya dalili ambazo si nzuri kwa mwanamke aliye mjamzito kama zinavyoelezwa na bingwa wa masuala ya uzazi na magonjwa ya kina mama Dr. Mashavu Khalid Othman.
