MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage, amesema hawezi kuitisha mkutano mkuu wa dharura alioelekezwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuwa shirikisho hilo halina mamlaka ya kufanya hivyo.
"Kwanza hawa watu walionisimamisha wanasema ni uamuzi ya kamati ya utendaji, hii si kweli kile hakikuwa kikao cha kamati ya utendaji bali ni kikao cha kawaida tu kama kikao cha harusi," alisema Rage.
"Katiba ya Simba ibara ya 28 (1) kuanzia a, b, c mpaka d inasema wazi kwamba, maana ya kamati ya utendaji ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe saba. Kama ikitaka kuketi, Mwenyekiti ndiye mwenye jukumu la kuitisha kikao au Makamu Mwenyekiti kwa ridhaa ya Mwenyekiti kama akiona kuna ulazima wa kufanya hivyo," alisema Rage.
Rage alisema Katiba ya Simba
inamlazimisha Mwenyekiti kuitisha vikao vinne kwa mwaka, yaani kimoja
kila baada ya miezi mitatu, lakini yeye ameshaitisha vikao 12 ndani ya
mwaka huu.
"Nilipeleka barua yangu TFF kuelezea uhuni huu uliofanywa na hawa watu, lakini wao hawakutoa tamko lolote la kulaani hiki kinachoitwa mapinduzi na badala yake wanalazimisha mimi niitishe mkutano, Katiba ya Simba haisemi hivyo," alisema Rage.
"Ibara ya 22 ya Katiba ya Simba inayoelezea kuhusu Mkutano Mkuu inasema mwenye wajibu wa kufanya hivyo ni Mwenyekiti kwa kushirikiana na kamati ya utendaji kama anaona inafaa. Hapo unaona nani mwenye mamlaka hayo sasa hili la maelekezo ya TFF linatoka wapi?" Alihoji Rage.
"Wakati uchaguzi wa TFF ulipoingia katika mgogoro kwa baadhi ya wagombea, Fifa (Shirikisho la Soka la Kimataifa) iliamuru uchaguzi huo ufanyike baadaye lakini si kwa kuipangia TFF kama wanavyofanya kwetu sisi.
"Najua kuna kiongozi mmoja aliyekuwa Simba na sasa yupo TFF ndiye anayeniandama na kunichafua kila mahali. TFF niliwapelekea barua ya mambo yote haya na ilipaswa kamati ya maadili ipitie lakini badala yake kamati ya utendaji ndiyo iliyofanya kazi hiyo, hakuna kitu kama hicho. Sasa wakiendelea kulazimisha mkutano mimi nitajiuzulu.
"Kwa mamlaka niliyonayo, namtangaza ndugu Michael Wambura kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba kwani Malkia wa Nyuki (Rahma Al Kharoos) aliniomba kutoka katika kamati hiyo.
"Badala yake nami nilimuomba Malkia wa Nyuki aingie katika baraza la wadhamini na kuanzia sasa yeye atakuwa mmoja wa wajumbe wa baraza la udhamini na jina lake litathibitishwa na mkutano mkuu hapo baadaye."
Katika hali isiyo ya kawaida, Rage alikataa maswali kutoka kwa waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wake.
"Sitaki swali lolote kutoka kwenu na anayetaka kuandika aende kuandika na asiyetaka aache, najua wengi wenu mnatumiwa na hawa watu," alisema Rage bila kufafanua wala kutaja jina la watu anaodai wanawatumia waandishi.
Rage anaondoka nchini leo Jumatatu kwenda London, Uingereza akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya hesabu za serikali ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwanaspoti lilipowasiliana na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura alisema; "Ni halali kwa kamati ya utendaji kupitia barua ya Rage kwa kuwa ile ya maadili haikuwa imeundwa na kuhusu kukaidi kwake kuitisha mkutano sisi tunangoja siku 14 zipite halafu utaona tunafanya kitu gani leo (jana Jumapili) ndiyo kwanza siku ya pili."
Alipotafutwa na Mwanaspoti, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang'are 'Mzee Kinesi' hakutaka kusema lolote.
Chanzo:Mwanasport.