Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Kenya yaongoza kwa ufisadi

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
Kenya yaongoza kwa ufisadi
Na Mwandishi wetu, Nairobi  (email the author)

Kenya Yaongoza kwa ufisadi kati ya nchi 107 ambako utafiti huo ulifanyika,jambo ambalo limewasikitisha wakenya
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Transparency International, Kenya imeshika nafasi ya nne kwa ufisadi ikiwa ni  miongoni mwa nchi 107 ambako utafiti huo ulifanywa.

Ripoti hiyo ilibaini kwamba Wakenya saba kati ya 10 waliohojiwa walisema wamewahi kutoa hongo maishani mwao ili waweze kupata huduma moja hadi nane kati ya zilizochunguzwa.

Kulingana na utafiti huo, maofisa wa polisi ndio waliopatikana kuwa mafisadi zaidi nchini wakifuatiwa na wabunge, vyama vya kisiasa, mahakama na wafanyakazi wa Serikali.

Wakenya wengi walisema vyombo vya habari, mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za kidini hazina ufisadi mwingi.

Nchi fisadi zaidi duniani ni Sierra Leone ambako asilimia 84 ya watu waliohojiwa walikubali kwamba wametoa hongo. Sierra Leone inafuatwa na Liberia (asilimia 75) na Yemen (asilimia 74).

Nchi ambazo zilipatikana kuwa na ufisadi finyu ni Finland, Japan, Australia, Denmark, Uhispania, Canada, Ureno, Uruguay, Norway, New Zealand, Korea Kusini na Malaysia ambako watu zaidi ya 95 kati ya 100 waliohojiwa walisema hawajaona ufisadi wowote nchini mwao.

Katika eneo la Afrika Mashariki, Kenya ndiyo nchi fisadi zaidi ikifuatwa na Uganda (asilimia 61) na Tanzania (asilimia 56). Kulingana na utafiti huo ambao watu 114,000 walihojiwa, Rwanda ilipatikana kuwa na ufisadi mdogo zaidi katika eneo la Afrika Mashariki. Raia 13 pekee kati ya 100 wa nchi hiyo walikubali mwamba wametoa hongo. 

Ufisadi ulipatikana kukithiri zaidi barani Afrika. Baadhi ya nchi fisadi zaidi Afrika ni Zimbabwe, Msumbiji, Libya na Cameroon (zote zikiwa na asilimia 62) na Nigeria (asilimia 44).
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top