Chuo cha mafunzo ya ufundi nchini tanzania (VETA) kilichopo kata ya kongowe, wilaya ya kibaha, mkoa wa pwani kinakabiliwa na changamoto ya vijana wazawa kukosa mwamko wa kuchangamkia fursa zilizopo katika eneo lao, ambazo fursa mojawapo ni kujiunga na chuo hicho ili kujikomboa kimaendeleo.
mbali ya changamoto hiyo, pia kwa upande wa wanafunzi wa kike, wanadaiwa kujitokeza kwa uchache zaidi. hali inayosababisha kukwamisha mipango na jitihada za serikari za kutaka kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira mkoani hapo.
akizungumza kwa niba ya mkuu wa chuo hicho, peniens nyoni, alisema hadi sasa katika kila darasa la ufundi kati ya wanafunzi 30 wasichana ni wawili pekee. nyoni anaendelea kusema kwamba, mbali na vijana hao kutojitokeza kwa wingi katika kujiunga na mafunzo chuoni hapo, hata wale waliojiunga hawana maudhurio mazuri,
kutokana na kutoloka nyakati za vipindi na wengine kuacha mafunzo kabisa, huku wanafunzi wanao toka mikoa ya mbali wakiendelea kufanya vyema zaidi kuliko wazawa.
diwani wa kata ya kongowe, sloom bagumesh, aliwaasa vijana kujitambua ikiwa ni pamoja na kutumia fursa zilizopo katika mapambano ya kujikwamua na umaskini.