Swali hili nalielekeza moja kwa moja mpaka kwako ewe msomaji wangu.
Ivi nchi kama Tanzania kukosa Shirika mbadala la kuzalisha umeme, ndo chanzo cha TANESCO kuvimba vichwa na kuanza kutupandishia bei za matumizi ya umeme???
Nauliza ivi kwa sababu moja kubwa ya msingi. Ivi majuzi Shirika la umeme tanzania Tanesco, lilitangaza kupanda kwa bei ya umeme. Nampaka sasa tayari viwango vya umeme mitaani vimeanza kubadilika kutoka katika hatua ya zamani na kushuka kwa idadi ya units ukilinganisha na ilivyokuwa hapo awali.
Cha kushangaza zaidi nipale unapoenda kununua umeme katika mashine za MAX-MALIPO, apo ndo utatamani kulia kabisa. Zamani kabla ya mabadiliko haya, ulikuwa ukienda kununua umeme wenye thamani ya Tsh.5, 000/= ulikuwa unapata 18 unit's iyo ni kwenye vituo vyote. Iwe ni kwenye max malipo au kwenye vituo vya kuuza ruku vilivyo alalishwa na shirika la umeme tanesco.
Ila baada ya katangaza mabadiliko haya kwa sasa ukienda kununua umeme wenye thamani ile ile ya Tsh 5, 000/= unapata 13 unit's. Sasa je kwa style hii tutafika kweli??????????????????Au ndo ile ya Ali mpya, nguvu zaidi na kasi ya ajabu??????