Mimi kwa jina naitwa Mosesi, ni mkazi wa mkoa wa katavi, umli wangu ni miaka 29. nina mpenzi wangu anaitwa Aisha. nimedumu naye kwa mda mrefu sana, kama miaka miwili na nusu hivi, tumepanga mambo mengi mazuri sana juu ya uhusiano wetu baina yangu mimi na yeye. ikiwa moja ya mipango hiyo ni kufunga ndoa pamoja.
lakini chakushangaza nipale familia yake wanapo amua kusema kwamba kama anataka kuoana na mimi ni lazima mimi nikabadili dini na kuwa mwislamu kama yeye. Jambo hili linaniumiza kichwa sana kiasi kwamba mpaka nakosa usingizi saazingine. Lakini kwa upande wake yeye Aisha yupo tayari kuoana na mimi ingawa itambidi kubadili dini na kunifuata mimi kama mkristo.
nimekaa na kuwaza sana juu ya mada hii, lakini majibu niliyopata naona kama hayajitosherezi, nikaona ni vyema niombe msaada wa kimawazo kutoka kwako ewe msomaji na mfuatiliaji wa habari kwa kupitia kwenye blog hii ya rafiki yangu.
Tafadhari naomba ushauri kutoka kwako, nifanye nini mpaka nitimize ndoto yangu juu ya binti huyu?? Kwaleo nihayo tu, nakutakia siku njema na Mungu akubariki.
Ameni
Jiunge na mi kwa kubonyeza kwenye link zifuatazo chini ili kupata habari mpya zaidi.
FACEBOOK >>> TWITTER >>> MATUKIO KWA NJIA YA SAUTI
