Nina mpenzi wangu anaitwa jasmini nipo nae chuo kimoja kasoro kozi zetu ndio tofauti.
Mimi nimepanga nje kidogo ya chuo yani naishi gheto na nikawaida yake yeye kuja kunitembelea anavyotaka pia kiukweli nampenda sana na yeye analijua hilo.
Kiukweli nina malengo nae ya kumuowa japo tuna tofauti za kidini ila huwa tukiliongelea hili anaonekana kama ni muelewa.
tatizo lake kazi zote ananiachia mimi hata zile ndogo ndogo na kama akiamua kufanya basi itakuwa nyimbo hata wiki nzima.
tatizo lake kazi zote ananiachia mimi hata zile ndogo ndogo na kama akiamua kufanya basi itakuwa nyimbo hata wiki nzima.
Pia kidogo anatishia tuachane hata kama hamna baya ambalo nimemfanyia ili nimpigie magoti.Anaweza akawa amelala akaniamsha nioshe vyombo au niweke chai jikoni katika gesi bila ya kubisha namfata anavyotaka ila tusije kugombana tu.
Swala hata kama mpenzi wako hana uwezo kifedha ndio umnyanyase kiasi hiki jamani?! Hivi kuna mapenzi ya dhati hapa au nibora niachane nae tu nijue moja kuliko kuzalilishwa kila siku,hebu nipeni jibu wadau wangu...
