Marehemu Sultan Sikilo, wa kwanza na picha ndogo (kulia) mstari wa mbele akiwa na wachezaji wenzake wa kikosi cha kwanza cha Taswa Fc, katika moja ya mchezo wa timu hiyo enzi za uhai wake. Mechi hii ilikuwa ni kati ya Tswa Fc na Taswa Uganda mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam, mwaka 2009.
Na Mwandishi Wetu, DarMWEKA Hazina wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na mchezaji wa timu ya Waandishi wa Habari za Michezo TASWA Fc, Sultan Sikilo, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitli ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kufuatia maladhi ya Homa ya Ini yaliyokuwa yakimsumbua.
Akizungumza na mtandao huu, Katibu wa TASWA, Amir Mhando alisema kuwa, Sikilo alifikishwa hospitalini hapo ambako umauti umemfika akitokea hospitali ya Temeke, Dar es Salaam, Alhamisi ya wiki hii.
“Ndugu yetu aligundulika ana matatizo ya homa ya ini siku ya Alhamisi katika hospitali ya Temeke na akahamishiwa Muhimbili, ambako umauti umemfika,”amesema Mhando.Aidha, Mhando amesema kuwa msiba wa marehemu Sultan upo nyumbani kwa wazazi wake Mbagala Maji Matitu na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Saa 9:00 Alasiri eneo la Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam. Mungu aiweke roho ua marehemu Sultan mahali pema peponi. Amen.
