Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

CHANZO CHA WANAFUNZI KUFERI MITIHANI YAO.

Naomba nikushirikishe na wewe pia kwamba kuna mambo mengi na mazuri ndapi ya picha iliyopo hapo chini ibofye uone.
IMEBAINIKA kuwa chanzo cha ufaulu hafifu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika Mkoa wa Pwani kinasababishwa na walimu wengi kukaa mbali na vituo vyao vya kazi.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Idara ya Elimu mkoani Pwani, umebaini kuwa asilimia kubwa ya walimu wanakaa mbali na vituo vyao vya kazi, hivyo kushindwa kufundisha vipindi vyote vya masomo kwa muda unaotakiwa.

Akiwasilisha taarifa ya utafiti kwa wadau wa elimu wa mkoa huo katika kikao kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, Ofisa Elimu wa mkoa huo Wariambora Nkya, alisema kuwa baadhi ya walimu wanaishi kilomita 15 kutoka katika vituo vyao vya kazi.

Nkya alisema kuwa hali hiyo imesababisha walimu hao kuchelewa kuripoti shuleni na kuwahi kuondoka kabla ya muda wa kazi, hivyo kushindwa kufundisha baadhi ya vipindi.

Aliongeza kuwa tatizo hilo limesababisha wanafunzi wengi kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao.

Aidha, utafiti huo pia umebaini kushuka kwa kiwango cha elimu katika mkoa huo, hali inayosababishwa na baadhi ya wazazi kutokuwa na mwamko wa kuchangia katika shughuli mbalimbali za elimu.Nkya pia alisema kuwa zipo baadhi ya shule katika Wilaya ya Mkuranga, wanafunzi wake hawajafundishwa masomo ya uraia, haiba na michezo kwa wiki 14 tangu shule zifunguliwe.

Utafiti huo umebaini pia shule nyingi zilizopo pembezoni mwa halmashauri kuwa na uhaba wa walimu, hali inayochangia uzoroteshaji wa ufundishaji kutokana na kuwa na wanafunzi wengi tofauti na idadi ya walimu waliopo.
Utafiti huo ulifanyika baada ya agizo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, ili kujua kinachosababisha mkoa huo kuwa nyuma katika suala la elimu.
Usikose kuangalia Movies mbalimbali kutoka kila kona ya dunia, bofya kwenye picha iliyopo hapo chini kuona izo muvies
Nobody is a total failure if he dares to try to do something worthwhile. Tough times never last, but tough people do. The place broke up with applause. Those thirty - five hundred farmers who had lost hope and had battled depression found that hope.

Share habari hii kadri uwezavyo.

Contact us on mutalemwa.oesmo@gmail.com. Powered by Blogger.
© Copyright Mutalemwa Blog
Back To Top